• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yakosoa kauli ya kutengana kwa uchumi wa China na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-07-25 20:40:27

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, kauli inayosema uchumi wa China na Marekani unatengana ni kinyume na utaratibu wa uchumi wa soko, matumaini ya makampuni, na neema ya wananchi wa nchi hizo mbili, na pia itaathiri mnyororo wa uzalishaji wa kimataifa na uchumi wa dunia.

  Bw. Gao amayesema hayo kwenye mkutano na wanahabari alipojibu swali kuhusu baadhi ya wamarekani kusema uchumi wa Marekani na China unatengana.

  Bw. Gao amesema katika miaka 40 tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi, uchumi wa nchi hizo mbili umefungamana kwa kina, na hali hii imewanufaisha wananchi wa nchi hizo mbili na watu wa dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako