• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa mafunzo ya wakunga wasaidizi wa Afrika wasaidia kuboresha afya ya wajawazito, akina mama waliojifungua na watoto

    (GMT+08:00) 2019-07-26 18:59:35

    Awamu ya pili ya darasa la mafunzo ya wakunga wasaidizi wa Afrika "Malaika wa Maisha" inaendelea katika Chuo Kikuu cha Matibabu cha Wenzhou kilichopo mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, na imewashirikisha wanasemina 25 kutoka nchi za Afrika zikiwemo Tanzania, Ghana, Uganda, Rwanda, Nigeria na Zambia.

    Mshiriki kutoka Tanzania Mwacha Happiness Tibruce anayepata mafunzo ya kuwahudumia wajawazito na watoto wachanga katika Chuo Kikuu cha Matibabu cha Wenzhou amesema, anatarajia kurudi nyumbani na mambo yote aliyojifunza katika chuo hicho ili kuchangia katika afya ya akina mama na watoto. Anasema,

    "Katika nchi yetu baadhi ya wajawazito wanashindwa kujifungua hospitalini kwani nyumba zao ziko mbali na hospitali. Na kama watu wengi wana elimu ya ukunga, wanaweza kuwasaidia wajawazito hao na kupunguza hatari zinazoweza kutokea wakati wa kujifungua."

    Mradi wa mafunzo kwa wakunga wasaidizi wa Afrika ulizinduliwa tarehe 20, Agosti mwaka jana, na unalenga kutoa mafunzo ya kusaidia kujifungua kwa wanafunzi wa Afrika wanaosomea hapa China ambao hawasomei udaktari, kueneza elimu ya matibabu ya akina mama na watoto kwa vijana wenye ujuzi wa Afrika, na kutarajia kuboresha kiwango cha afya kwa wajawazito, akina mama waliojifungua, na watoto wachanga. Awamu ya kwanza ya mradi huu ilihusisha watu 15 kutoka Afrika.

    Mkuu wa kitivo cha huduma cha Chuo Kikuu cha Matibabu cha Wenzhou na naibu mkurugenzi wa hospitali ya kwanza ya chuo kikuu hicho Bw. Lu Zhouqiu amesema, hii ni hatua ya kivitendo kwa chuo kikuu chao kuitikia pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika, na pia inaimarisha utoaji mafunzo ya elimu na uandaaji wa watu wenye ujuzi wa udaktari kwa nchi za Afrika. Anasema,

    "Siku zote tunafikiria jinsi ya kutumia ipasavyo nguvu ya chuo kikuu chetu na kuboresha huduma za matibabu katika nchi za Afrika. Tunatarajia kuwa kwa kupitia mradi huu wa kutoa msaada na mafunzo ya ukunga, tunaweza kusaidia kuboresha kiwango cha afya kwa wajawazito, akina mama waliojifungua na watoto wachanga katika nchi za Afrika."

    Ripoti iliyotolewa na Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa UNFPA na Shirika la Afya Duniani WHO imesema, kiwango cha vifo vya wajawazito katika nchi za Afrika kimezidi asilimia 8, ambayo imezidi kiwango cha wastani cha dunia cha asilimia 0.2. Wakunga wanachukuliwa kama "mlinzi mtakatifu" na wamefanya kazi kubwa katika kupunguza kiwango cha vifo vya wajawazito, akina mama waliojifungua na watoto wachanga, na kuboresha afya zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako