• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kuwa mwenyeji wa kongamano la miundo mbinu Afrika

    (GMT+08:00) 2019-07-26 19:26:23

    Waziri wa fedha wa Uganda Bw Gabriel Adjedra amesema Uganda itakuwa mwenyeji wa Kongamano litakalowaleta pamoja wadau wa sekta ya kibinafsi na ile ya Umma litakalokuwa likilenga maendeleo ya Miundo mbinu. Adjedra amesema kongamano hilo litatoa jukwaa kwa serikali za Afrika kutangaza miradi yake pamoja na sekta ya kibinafsi ambapo watapata fursa ya kutambua miradi ya miundo mbinu wanayoweza kuwekeza.Hata hivyo macho yataelekezwa zaidi kwa miradi ya miundo mbinu ya Uganda haswa Nishati, afya, kilimo, ajira na uchukuzi. Kongamano hilo la siku tatu linatarajiwa kufanyika kati ya Septemba 16-18. Kauli mbinu ya Kongamano hilo ni "Mambo makubwa ya ya Afrika katika siku zijazo" . Kongamano hilo linaandaliwa na Idara ya umoja wa kimataifa kuhusu uchumi pamoja na serikali ya Uganda. Jumla ya wataalam wa mambo ya miundo mbinu 50 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako