• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Ufilipino zakubaliana kulinda amani na utulivu wa Bahari ya Kusini ya China

    (GMT+08:00) 2019-07-26 19:32:03

    China na Ufilipino zimefanya majadiliano ya awamu ya 22 ya kidiplomasia na kukubaliana kulinda mwelekeo mkuu wa amani na utulivu katika Bahari ya Kusini ya China.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying, amesema majadiliano hayo ni ya kwanza baada ya nchi hizo mbili kuinua ngazi ya uhusiano wao kuwa wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote mwaka jana, na nchi hizo zimejadili kwa kina uhusiano wao, ushirikiano katika sekta mbalimbali na masuala ya kimataifa na kikanda, na pia zimefikia maoni ya pamoja katika kulinda amani na utulivu wa Bahari ya Kusini ya China.

    Bibi Hua ameongeza kuwa China na Ufilipino pia zimesisitiza kulinda ujirani mwema kati yao, kuimarisha ushirikiano kuhusu "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kuwa majirani wema, marafiki wazuri na wenzi wazuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako