• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaanza kutumia mbinu ya kutokomeza Malaria iliyotumika China kutokomeza ugonjwa huo mikoa ya Kusini

    (GMT+08:00) 2019-07-27 17:33:26

    TANZANIA imeanza kutekeleza mradi wa kutokomeza malaria kwenye mikoa ya kusini kwa kutumia mbinu iliyotumika kuutokomeza nchini China.

    Imeelezwa kuwa mafanikio ya awamu ya kwanza ya mradi huo umepunguza maambukizi ya malaria kutoka asilimia 24.7 hadi asilimia 4.7 ambayo ni chini ya kiwango cha maambukizi kitaifa cha asilimia 7.3.

    Mbinu hiyo ya kitaalamu inahusisha kufuatilia wagonjwa wanaotibiwa malaria kwenye vituo vya afya kisha kufanya upimaji kwenye vitongoji vya makazi walikotoka wagonjwa hao.

    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu waziri wa afya wa China, Li Bin juzi wali walikagua shughuli za mradi wilayani Rufiji, Pwani.

    Ummy alipongeza mafanikio ya awamu ya kwanza ya mradi huo ambao ulipunguza maambukizi ya malaria kutoka asilimia 24.7 hadi asilimia 4.7 ambayo ni chini ya kiwango cha maambukizi kitaifa cha asilimia 7.3.

    Utelezaji wa mradi huo wa miezi 18 unatokana na matokeo mazuri ya awamu ya kwanza. Kupitia mbinu hiyo ya kufuatilia wagonjwa wanaotibiwa malaria kwenye vituo vya afya, maambukizi ya malaria yamepungua kwa asilimia 68.

    "Tunashukuru sana ushirikiano na serikali ya China kwenye mradi huo. Bila shaka tuna sababu ya kupanua maeneo yanayofaidika na mradi huo kufikia wilaya zaidi na mikoa mingine ya kusini," anasema Ummy.

    Naye,Naibu waziri wa afya wa China, Li alipongeza ushirikiano ulioonekana katika awamu ya kwanza ya mradi na kuahidi kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kupambana na malaria.

    China ilitokomeza malaria kutoka wagonjwa milioni 30 hadi kutokuwa na mgonjwa hata mmoja mwaka 2017.

    "Tuko tayari kushirikisha Tanzania kutumia mbinu tulizotumia kufikia mafanikio hayo," alisema Li .

    Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Ritha Njau, akizungumza kwa niaba ya mwakilishi mkazi, anasema shirika litafanya kazi na serikali kuhakikisha mradi huo unatelezwa kwa viwango vya juu.

    Mradi huo unaotumia mbinu shirikishi kwa wadau, WHO imesema itahakikisha unafanyika kwa kiwango cha juu. Tanzania imefanikiwa kupiga hatua kupunguza vifo vya malaria kutoka vifo 20 kwa kila watu 1000 hadi vifo tisa kwa kila Watanzania 1000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako