• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya mkoa maalumu wa Hong Kong yalaani maandamano haramu yaliyofanyika eneo la Yuen Long

    (GMT+08:00) 2019-07-29 08:10:40

    Msemaji wa serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong nchini China amelaani vikali maandamano haramu yaliyofanyika Jumamosi kwenye eneo la Yuen Long na kuzusha vurugu za kimabavu.

    Amesema serikali imesikitishwa na ushiriki wa wakazi wa Hong Kong kwenye maandamano hayo licha ya kupigwa marufuku na kupingwa na serikali. Ameongeza kuwa baadhi ya waandamanaji wenye itikadi kali walivamia mistari ya ulinzi iliyowekwa na askari polisi, kuharibu magari ya polisi na kufunga barabara. Serikali ya Hong Kong inalaani vikali vitendo vya waandamanaji hao vya kuhujumu utulivu wa kijamii na kukiuka sheria. Amesisitiza kuwa polisi wa Hong Kong watawachukulia hatua waandamanaji walioshiriki kwenye vitendo hivyo vya kimabavu.

    Kwa mujibu wa polisi, wanaume 11 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 68 walikamatwa kwenye operesheni ya kuwatawanya waandamanaji hao, kwa tuhuma za kushiriki kwenye maandamano haramu, kumiliki silaha na kushambulia polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako