• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KIKAPU: DRC yanyakua ubingwa wa kikapu Afrika, yaichapa Kenya.

  (GMT+08:00) 2019-07-29 08:42:42

  Timu ya taifa ya kikapu ya DR Congo imetwaa ubingwa wa kikapu wa Afrika baada ya kuishinda Kenya kwa vikapu 82 kwa 61 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Bamako Mali.

  Mzunguko wa tatu DRC iliongoza kwa vikapu 29 kwa 10 kabla ya DRC kuongoza mzunguko wa nne kwa vikapu 17 kwa 14. Maxi Shamba wa DRC alifunga vikapu 20 na kufanikisha Rebound saba. Naye Tylor Ongwae wa Kenya alifunga vikapu 21 katika mchezo huo.

  Angola imemaliza ya tatu katika mashindano hayo kwa kuishinda Morocco kwa vikapu 88 kwa 71. Mashindano hayo yalishirikisha timu 12 huku Afrika Mashariki ikiwakilishwa na Kenya pekee.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako