• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sekta tatu za ukuaji wa uchumi zachangia asilimia 16.1 kwa pato la ndani GDP nchini China

  (GMT+08:00) 2019-07-29 18:30:16

  Idara ya Takwimu ya China imetangaza kuwa, kutokana na mahesabu ya hatua ya mwanzo, sekta tatu za ukuaji zimechangia asilimia 16.1 kwa pato la ndani GDP nchini China mwaka jana, kiasi ambacho kimezidi kwa asilimia 0.3 ikilinganishwa na mwaka 2017. Wataalamu wanaona kuwa hali hii imeonesha mabadiliko ya msukumo wa ukuaji wa uchumi, na muundo wa uchumi wa China unazidi kuboreshwa.

  Sekta hizo tatu zinahusisha mambo ya kilimo cha kisasa, misitu na ufugaji, viwanda vya kisasa vya utengenezaji, shughuli za nishati za aina mpya, kubana matumizi ya nishati na ulinzi wa mazingira, utoaji wa huduma za mtandao wa Internet na TEHAMA, utoaji wa huduma za teknolojia za kisasa na viwanda vya uvumbuzi.

  Naibu mkurugenzi wa Kamati ya sera za uchumi iliyo kwenye Taasisi ya utafiti kuhusu sera za sayansi ya China Bw. Xu Hongcai anaona kuwa, kuongezeka kwa thamani ya sekta hizo tatu za ukuaji wa uchumi kumeonesha mabadiliko ya msukumo wa ukuaji wa uchumi, akisema:

  "Tumegundua kuwa, msukumo wa zamani wa kuhimiza uchumi umepungua kwa dhahiri. Tunachotakiwa kufanya ni kutafuta msukumo mpya wa ongezeko la uchumi kupitia kuongezeka uwekezaji katika utafiti na uendelezaji, na kuboresha muundo wa uchumi. Na sekta hizo tatu za ukuaji wa uchumi zimeonesha msukumo huo mpya wa ukuaji wa uchumi katika siku za baadaye."

  Mwaka 2018 thamani ya sekta tatu mpya za ukuaji wa uchumi katika viwanda vya utengenezaji iliongezeka kwa kasi zaidi, na kasi ya ukuaji wake imefikia asilimia 15.1, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.2 kuliko mwaka 2017 wakati kama huu. Bw. Xu Hongcai anaona kuwa, uchumi wa China utapata maendeleo makubwa zaidi, akisema:

  " Watu wataweza kuona kuwa, thamani ya sekta tatu mpya za ukuaji wa uchumi itachukua nafasi kubwa zaidi, na kasi ya ongezeko lake itazidi wastani wa ongezeko, na uchumi wa China utapata ukuaji wa sifa bora, hali ambayo itawanufaisha wananchi, na kuzidi kuhimiza uchumi wa China kupata maendeleo endelevu."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako