• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatumia dola bilioni 1.25 za kimarekani kuunga mkono watu wanaohitaji msaada

  (GMT+08:00) 2019-07-29 18:56:13

  Wizara ya mambo ya kiraia ya China imesema, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa Machi mwaka huu China imetumia dola bilioni 1.25 za kimarekani kuunga mkono watu wanaokabiliwa na matatizo maalumu.

  Watu zaidi ya milioni 4.78 wanaoishi katika hali ngumu, ikiwa ni pamoja na wazee, wasiojiweza, watoto ambao hawana uwezo wa kufanya kazi, kutokuwa na mapato na kutokuwa na watu wa kuwategemea. Kati ya watu hao wanaohitaji msaada, karibu milioni 4.5 wanatoka kwenye maeneo ya vijijini, huku wengine laki 2.86 wakitoka kwenye maeneo ya mijini.

  Wakati huohuo, hadi kufikia mwishoni mwa Mei mwaka huu dola bilioni 9.11 za kimarekani zimetengwa kama ruzuku kwa watu milioni 44 ambao milioni 9.4 kati yao wanatoka kwenye maeneo ya mijini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako