• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: CAF yateua waamuzi tayari kwa michuano ya Klabu bingwa na Kombe la Shirikisho.

    (GMT+08:00) 2019-07-30 07:42:49
    Shirikisho la soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi wanne na makamishna wawili toka Tanzania kusimamia mechi za ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho barani Afrika.

    Elly Sasii atasimama kati kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Aigle Noir ya Burundi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya mchezo utakaopigwa uwanja wa Prince Louis Rwegasore Burundi Agosti 11 mwaka huu.

    Naye Khadil Abdallah ameteuliwa kuwa kamishna wa mchezo wa kombe la shirikisho kati ya Proline FC ya Uganda na Master Security Service ya Malawi utakaochezwa uwanja wa Kampala Star Times Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako