• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutekeleza mipango ya kuhimiza afya ya wazee

    (GMT+08:00) 2019-07-30 17:00:11

    China ni nchi yenye idadi kubwa zaidi ya wazee duniani, vilevile ni moja kati ya nchi ambayo idadi hiyo inayoongezeka kwa kasi zaidi, na hali ya afya ya wazee nchini China pia si ya kuridhisha. Kutokana na hali hii, China imepanga kutekeleza hatua za kuhimiza afya ya wazee, ili kuinua kiwango cha afya na kuboresha maisha yao.

    Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018, idadi ya wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60 nchini China ilifikia milioni 249, ikichukua asilimia 17.9 ya idadi ya jumla ya watu, huku idadi ya wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 65 ikifikia milioni 167, na kuchukua asilimia 11.9 ya idadi ya jumla ya watu. Mkurugenzi wa Idara ya afya ya wazee kwenye Kamati ya afya ya taifa Bw. Wang Haidong ameeleza kuwa, hali ya jumla ya wazee nchini China sio ya kuridhisha. Anasema:

    "Takwimu zimeonesha kuwa, idadi ya wazee wenye magonjwa sugu imezidi milioni 180, wale walio na zaidi ya aina moja ya magonjwa sugu imefikia asilimia 75, idadi ya wazee wasioweza kuishi peke yao imefikia milioni 40. Wakati huo huo, takwimu zimeonesha kuwa, mwaka 2018, wastani wa maisha ya wazee ni umri wa miaka 77, lakini maisha ya wazee wenye afya njema ni miaka 69 hivi, hali ambayo imeonesha kuwa wazee wanaishi wakiwa na magonjwa kwa miaka minane."

    Mipango ya afya ya China ya mwaka 2019-2030 iliyotangazwa hivi karibuni itakamilisha utaratibu wa utoaji wa huduma za afya kwa wazee, kuboresha sera za utunzaji wa wazee nyumbani na mitaani, ili kujenga mazingira mazuri kwa wazee na kutimiza lengo la kuwawezesha wazee kuishi na afya. Bw. Wang Haidong anasema:

    "Ili kutekeleza mipango ya kuhimiza afya ya wazee, inapaswa kueneza ujuzi mbalimbali kwa wazee hao ikiwemo lishe, mazoezi ya kujenga afya, upimaji wa afya mara kwa mara, usimamizi wa afya ya mwili na kisaikolojia, na matumizi mwafaka ya dawa. Pia kukamilisha utaratibu wa utoaji wa huduma za afya kwa wazee, kukamilisha sera za utunzaji wa wazee nyumbani na mitaani, kutafuta mfumo wa bima ya matunzo ya muda mrefu, ili kujenga mazingira mazuri kwa wazee na kuwafanya waishi kwa afya njema."

    Mbali na hayo, mipango hiyo imefafanua kuwa, mashirika ya matibabu yatarahisisha njia kwa wazee kusajiliwa. Serikali inapaswa kutoa elimu kwa ajili ya ujuzi unaohusika, kutekeleza mipango ya kukinga maradhi ya moyo, na kutoa huduma ya maisha ya kawaida na saikolojia kwa wazee wenye umri mkubwa ambao wanaishi peke yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako