• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ronaldo atwaa tuzo ya Marca's Legend Uhispania, Shangwe kama lote

  (GMT+08:00) 2019-07-31 08:12:44

  Usiku wa Jumatatu mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo ambaye ni mshambuliaji wa bibi kizee wa Turin (Juventus) alitwaa tuzo ya Marca's Legend award nchini Uhispania inayotolewa kwa mwanamichezo aliyefanya mambo makubwa nchini humo.

  Kabla ya kutua Juventus, Ronaldo alichezea Real Madrid kwa miaka 9 akiifungia magoli 311 katika michezo 292. Ametunukiwa tuzo hiyo akifuata nyayo za mastaa kadhaa wa michezo mbalimbali ikiwemo soka.

  Wakati akikabidhiwa tuzo hiyo na rais wa Real Madrid Florentino Perez, mashabiki walisikika wakimtaka kiongozi huyo kumrejesha Ronaldo kukipiga tena kwenye klabu hiyo ya Madrid. Ronaldo alijikuta akitokwa na machozi mara baada ya mtoto mmoja kumweleza kuwa alijisikia vibaya sana alipomuona akiondoka Real Madrid na nyota huyo kujibu hata yeye pia ilikuwa hivyo hivyo na kutokwa na machozi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako