• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Bale aikacha safari ya Munich, mashabiki wataka atoe neno.

  (GMT+08:00) 2019-07-31 08:13:59

  Gareth Bale amejiondoa katika safari ya Real Madrid ya kwenda Munich kwa ajili ya shindano la kabla ya msimu kufuatia hatua yake ya pendekezo lake la kuhamia China ambalo halikufanikiwa.

  Wiki iliyopita, meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane alisema kuwa Bale mwenye umri wa miaka 30- alikuwa karibu kuihama klabu hiyo.

  Real ambao ni washindi wa ligi ya Uhispania mara 33 watacheza na klabu aliyoichezea zamani ya Bale, Tottenham Jumanne ijayo katika mechi ya ufunguzi wa mashindano yatakayozijumuisha Bayern Munich na Fenerbahce.

  Kiungo wa nyuma kushoto Danny Rose amejumuishwa katika kikosi cha Spurs, licha ya kuachwa kwenye safari ya michuano ya kabla ya msimu barani Asia ili atafute klabu mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako