• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema itashikilia kithabiti biashara ya pande nyingi

    (GMT+08:00) 2019-07-31 08:32:55

    Balozi mpya wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun ameahidi kuwa nchi hiyo itashikilia kithabiti biashara ya pande nyingi na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuchukua nafasi yake.

    Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York, Marekani, Balozi Zhang amesema China inapinga kithabiti vitendo vya upande mmoja na kujilinda, na kuongeza kuwa ushirikiano wa China katika Umoja huo uko katika mwanzo mpya.

    Akizungumzia baadhi ya maeneo ya ushirikiano huo, balozi Zhang amesema, China itashiriki kikamilifu katika majadiliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, usalama wa mtandao wa internet, mapambano dhidi ya ugaidi, na kuondoa silaha za nyuklia ili kutoa mchango wa China katika kukabiliana na changamoto hizo na kujenga jamii ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako