• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mipango ya kazi ya uchumi ya Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya CPC yahusisha hatua halisi na yenye ufanisi

    (GMT+08:00) 2019-07-31 16:49:41

    Idara ya Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imeitisha mkutano utakaotafiti hali ya uchumi kwa hivi sasa, na kuweka mipango kuhusu kazi ya uchumi katika nusu ya pili ya mwaka huu.

    Mkutano huo umeeleza kuwa, hivi sasa maendeleo ya uchumi wa China yanakabiliwa na changamoto mpya, huku shinikizo linaloukabili ukuaji wa uchumi likiongezeka, hivyo inapaswa kuongeza wazo la kukabiliana na hatari, na kubadilisha migogoro kuwa fursa nzuri ya kutumiwa na kushughulikia vizuri mambo yake yenyewe.

    Mkutano huo umesisitiza kushikilia msingi wa kuhimiza kazi za maendeleo kwa hatua madhubuti, kufanya mageuzi ya kimuundo, kushikilia mawazo mapya ya kujiendeleza, na kuhimiza maendeleo yenye sifa bora. Pia umeeleza kuwa, inapaswa kutekeleza sera imara ya fedha na zile zinazochochea ukuaji wa uchumi, na kuendelea kutekeleza sera za kupunguza utozaji wa kodi na bei ya bidhaa. Kuhusu soko la nyumba, mkutano huo umesisitiza kwa mara nyingine tena, kuwa jukumu la nyumba ni makazi, badala ya kuchuma pesa. Inapaswa kutekeleza utaratibu wa muda mrefu wa usimamizi wa nyumba, na kutangaza kwa mara ya kwanza kuwa, haipaswi kuchukua sekta ya nyumba kama mbinu ya kuchochea uchumi ndani ya muda mfupi.

    Mwanauchumi mwandamizi wa Benki ya Zhongyuan ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya kitaaluma ya Kituo cha kimataifa cha mawasiliano ya uchumi cha China Bw. Wang Jun anasema:

    "Kiini cha taarifa hiyo ni kutatua matatizo na masuala wanayoyakabili kwa njia ya mageuzi. Njia ya kushughulikia vizuri mambo yetu sisi wenyewe ni kuharakisha hatua ya kufanya mageuzi na ufunguaji mlango, badala ya kulegeza kupita kiasi sera za fedha. Ni muhimu kwetu kudumisha imani imara mbele ya hali na mazingira ya hivi sasa."

    Mbali na hayo, mkutano huo pia umedai kutafuta mustakabali wa mahitaji ya soko la ndani, kupanua mahitaji ya mwisho, kufungua kwa ufanisi soko la vijijini, kutuliza uwekezaji katika viwanda vya utengenezaji, na kuchukua hatua halisi kuunga mkono maendeleo ya viwanda vya watu binafsi.

    Bw. Wang Jun anasema: "Mipango ya kazi ya nusu ya pili ya mwaka huu itahusisha mambo halisi na yenye ufanisi zaidi, kwa mfano kutafuta mustakabali wa soko la vijijini, kupanua mahitaji ya matumizi, na pia umesisitiza kupanua matumizi kwa njia ya mageuzi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako