• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaikaribisha Marekani kuthibitisha na kuahidi kutoingilia mambo ya Hong Kong kwa njia yoyote

    (GMT+08:00) 2019-07-31 19:31:18

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani hivi karibuni imekanusha hoja kuwa nguvu ya nje ni nguvu inayofichwa nyuma ya hali ya Hong Kong. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema, kama Marekani itaweza kuthibitisha na kuahidi kutoingilia mambo ya Hong Kong kwa njia yoyote, China itakaribisha hatua hiyo.

    Wakati Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ikijibu swali kuhusu msimamo wa China kuhusu uingiliaji wa Marekani katika mambo ya Hong Kong, imesema inakataa hoja kwamba nguvu ya nje ni nguvu inayofichwa nyuma.

    Bi Hua amesema, kutokana na ripoti nyingi kutoka vyombo vya habari, kama tukiacha upendeleo, tutaweza kuona na kufanya uamuzi sahihi. Sasa Marekani inapaswa kutoa taarifa yenye udhati na uwazi kwa dunia. Na kama Marekani itaweza kuthibitisha na kuahidi kutoingilia mambo ya Hong Kong kwa njia yoyote, China itakaribisha hatua hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako