• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka pande mbalimbali za Sudan Kusini kutekeleza makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2019-07-31 19:43:49

    China imezitaka pande zilizosaini makubaliano ya amani ya Sudan Kusini mwezi Septemba mwaka jana, kuharakisha utekelezaji wa makubaliano hayo ili kukomesha mgogoro kwenye nchi hiyo.

    Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umesema kwenye taarifa iliyotolewa jana, kuwa China inaunga mkono juhudi za kurudisha amani na usalama nchini humo na kuwataka viongozi wa nchi hiyo kuweka maslahi binafsi pembeni, kwa ajili ya maslahi ya wasudan kusini wote.

    Mwambata wa ubalozi wa China mjini Juba Bw. Feng Bo amesema China inatumai pande mbalimbali zitaweka mbele maslahi ya umma, kujenga imani kuhusu amani, kutekeleza wajibu wao kwa amani, kuhimiza ufufuaji wa makubaliano ya amani, na kufikia amani ya kudumu haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako