• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China akutana na rais wa Colombia

  (GMT+08:00) 2019-07-31 19:47:52

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amekutana na rais Ivan Duque Marquez wa Colombia ambaye yuko ziarani nchini China.

  Bw. Li amesema Colombia ni mwenzi muhimu wa ushirikiano wa China katika kanda ya Latin Amerika. China inapenda kushirikiana na Colombia kuendelea kuimarisha maelewano ya kisiasa, kuimarisha kuunganisha mikakati ya maendeleo, kuzidisha ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali, ili kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika kiwango cha juu zaidi.

  Rais Duque amesema, Colombia inaipongeza China kwa maendeleo makubwa iliyopata katika miaka 70 iliyopita tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe, huku ikishikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na kutaka kudumisha mawasiliano ya ngazi mbalimbali na China.

  Habari nyingine zinasema spika wa Bunge la umma la China Bw. Li Zhanshu pia amekutana na rais Duque wa Colombia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako