• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Pendekezo watumiaji pufya sasa wafungwe gerezani

  (GMT+08:00) 2019-08-01 08:03:49

  Shirikisho la riadha Kenya (AK) limeahidi kuwaadhibu vikali na kukabiliana vilivyo na wanariadha wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa lengo la kujitafutia ufanisi katika mashindano mbalimbali.

  Mwenyekiti wa shirikisho hilo toka Nyanza kusini Peter Angwenyi amesema wanariadha watakaopatikana na hatia wanastahili kufungwa gerezani na kwamba kuwafungia kushiriki mashindano mbalimbali pekee haitoshi.

  Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, karibu wanariadha 50 wa Kenya wamehusishwa na matumizi ya dawa hizo akiwemo mshindi wa zamani wa mbio za Chicago na Boston, Rita Jeptoo na Jemima Sumgong aliyeibuka mshindi wa mbio katika Olimpiki za mwaka 2016 jijini Rio, Brazil.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako