• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: PUMA yaingia mkataba na Pep Guardiola wa Man City

  (GMT+08:00) 2019-08-01 08:03:36
  Kampuni ya vifaa vya michezo ya PUMA imekubali kuendeleza ushirika wake wa muda mrefu na Pep Guardiola baada ya kusaini mkataba mpya na kocha huyo wa mabingwa wa soka wa Uingereza.

  PUMA ilisaini mkataba wa kimkakati na Manchester City mwezi februari ikichukua nafasi ya kampuni ya NIKE katika harakati za kujiweka sawa baada ya kupoteza mkataba wa Arsenal ambayo imeingia ushirika na kampuni nyingine kubwa ya vifaa vya michezo ya Ujerumani ya Adidas.

  PUMA imesema, Guadiola atakuwa balozi wa chapa ya bidhaa zao. Guardiola anaungana na Sergio Aguero na David Silva kwenye orodha ya kampuni hiyo ambao ni mabalozi wa bidhaa zake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako