• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China azungumzia duru mpya ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-01 09:02:43

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amesema, China na Marekani zimeanzisha tena mazungumzo kuhusu suala la kiuchumi na kibiashara katika siku mbili zilizopita, ambapo zimetekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mjini Osaka, Japan, pia zimeitikia matarajio ya jumuiya ya kimataifa.

    Amesema duru mpya ya mazungumzo imefanyika kwa udhati, ufanisi na kwa njia ya kiujenzi, na anaamini kuwa pande hizo zikifuata moyo wa kuheshimiana, kufanya mazungumzo kwa usawa na kuzingatia mambo yanayofuatiliwa na upande mwingine, zitafikia makubaliano ya kunufaishana. Hayo yanaendana na maslahi ya China na Marekani, pia yanaendana na maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali.

    Bw. Wang Yi aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari baada ya kukutana na mwenzake wa Thailand huko Bangkok. Pia amesema, anapanga kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, na kwamba wataweza kubadilishana maoni kwa kina, kutatua migongano, kujadili ushirikiano, na kushirikiana kujenga uhusiano kati ya China na Marekani wenye msingi wa uratibu, utulivu na ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako