• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yadumisha mwelekeo wa kufanya mazungumzo kwa msingi wa usawa na kuheshimiana

    (GMT+08:00) 2019-08-01 17:21:22

    Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, raundi ya 12 ya Mazungumzo ya ngazi ya juu ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani ilikuwa wazi, ya kiujenzi na ya ufanisi mkubwa, na ilimalizika kama ilivyopangwa. Pia amesema, tangu tarehe 19 Julai, baadhi ya viwanda vya China viliuliza bei ya mazao mbalimbali ya kilimo kwa wauzaji wa Marekani, na kusaini awamu ya kwanza ya makubaliano. Pia ameeleza kuwa, baadhi ya viwanda vimetoa ombi la kufuta ushuru ulioongezwa kwa mazao hayo yanayoagizwa kutoka Marekani, na kamati ya kanuni za ushuru wa forodha kwenye Baraza la serikali la China inafanya tathmini na kushughulikia maombi hayo.

    Ni wazi kwamba si rahisi kupatikana kwa maendeleo hayo. Tokea mwezi Februali mwaka 2018 hadi sasa, China na Marekani zimefanya raundi 12 za mazungumzo, na kupata maendeleo makubwa huku zikikumbwa na changamoto mbalimbali.

    Historia na ukweli zimethibitisha kwa mara nyingine kuwa, hakuna mshindi katika vita ya biashara, na ushirikiano ni chaguo pekee sahihi kati ya pande hizo mbili. Kutokana na matokeo yaliyopatikana kwenye raundi hiyo ya mazungumzo, pande zote mbili hazikukwepa masuala nyeti na magumu, huku zikibadilishana maoni kuhusu masuala mengi yanayoyafuatiliwa kwa pamoja ndani ya muda mfupi, na kuonesha msimamo wa kuzingatia ufanisi katika ufumbuzi wa matatizo na mgogoro.

    Wakati huo huo pande hizo mbili pia zimejadili suala la manunuzi ya mazao ya kilimo, na China itaongeza uagizaji wa mazao ya kilimo kutoka Marekani kwa kufuata mahitaji ya soko la ndani, wakati huo huo, Marekani inahitaji kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uagizaji huo. Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili pia zimeamua kufanya raundi mpya ya mazungumzo mwezi Septemba nchini Marekani, ambayo yameonesha kuwa pande hizo zina matarajio ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi hizo mjini huko Osaka, Japan, na kuonesha msimamo wa kusaidiana katika kufanya ushirikiano.

    Tukikumbuka mchakato wa mazungumzo ya uchumi na biashara yaliyofanyika kati ya China na Marekani katika mwaka uliopita, mazungumzo mawili kati ya viongozi wa nchi hizo mbili katika kipindi muhimu, yamezuia kwa wakati kupamba moto kwa mgogoro wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili. Wakati huo huo, raundi mbalimbali za mazungumzo kati ya ujumbe wa uchumi na biashara wa pande hizo mbili yalikuwa magumu sana ambayo hayajawahi kuonekana katika historia ya mazungumzo ya uchumi na biashara duniani. Ndiyo maana ni vigumu kwa pande hizo mbili kurejea kwenye meza ya mazungumzo, na inapaswa kuzidi kusukuma mbele yapate maendeleo mapya.

    China, ikiwa kundi la pili lenye nguvu kubwa la kiuchumi duniani, siku zote inachukua mtazamo wa kuangalia siku za baadaye juu ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati yake na Marekani. Mikwaruzano na migogoro kati ya pande hizo mbili katika sekta za uchumi na biashara inahitaji kutatuliwa kupitia mazungumzo. Lakini ushirikiano unafanyika kwa kufuata kanuni, na China haitasalimu amri mbele ya masuala kuu. China siku zote inashikilia kushughulikia kwa makini mambo yake yenyewe, kuimarisha mageuzi kwa hatua madhubuti na kupanua ufunguaji mlango, na siku zote itakuwa mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako