• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mageuzi ya makampuni ya serikali ya China yamepata maendeleo makubwa

  (GMT+08:00) 2019-08-01 18:37:44

  Ofisi ya kikundi cha uongozi wa mageuzi ya makampuni ya serikali cha baraza la serikali la China, imesema tangu mwezi wa Agosti mwaka jana ilipoanza operesheni ya mageuzi ya makampuni ya serikali, operesheni hiyo imeendelezwa kwa kufuata matarajio na kupata maendeleo makubwa.

  Kwenye operesheni hiyo makampuni 400 hivi ya serikali katika ngazi ya taifa na mikoa, yanatekeleza majukumu ya mageuzi kutoka mwaka 2018 hadi 2020, ambayo yanalenga kutatua masuala magumu yanayoyakabili makampuni hayo na kuhimiza kazi mbalimbali za mageuzi.

  Naibu mkurugenzi wa ofisi hiyo Bw. Weng Jieming, amesema operesheni hiyo imekamilisha kazi 2524 za mageuzi ambazo ni asilimia 31.24 ya majukumu yote ya mageuzi hayo. Mageuzi ya mifumo ya umiliki wa hisa za makampuni ya serikali yameendelea vizuri, na utaratibu wa usimamizi wa wawakilishi wa makampuni umezidi kuboreshwa, huku mfumo wa uendeshaji wa soko ukikamilishwa na mifumo ya vizuizi dhidi ya vichocheo ukizidi kuboreshwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako