• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Nyota watatu Stars waondolewa, nafasi zao zachukuliwa na majembe mengine

    (GMT+08:00) 2019-08-02 07:53:30
    Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Etienne Ndayiragije amefanya mabadiliko katika kikosi cha timu hiyo kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi.

    Wachezaji walioondolewa katika kikosi kutokana na kuwa majeruhi ni David Mwantika, Aishi Manula na Ibrahim Ajibu ambao nafasi zao zimezibwa na Haruna Shamte pamoja na Mohamed Ally Yusuf wote wa Lipuli na Oscar Godfrey Masai wa Azam FC.

    Stars itamenyana na timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) jijini Nairobi Agosti 4 kwenye mchezo wa marudio wa kufuzu michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika Cameroon 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako