• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MASHINDANO YA MAGARI: Kuanza kutimua vumbi leo, Uganda

  (GMT+08:00) 2019-08-02 07:56:21

  Wakati mashindano ya 21 ya magari ya ubingwa wa Afrika yanatarajiwa kuanza leo na kuendelea wikiendi hii nchini Uganda, bingwa anayeshikilia taji hilo toka Uingereza Manvir Baryan tayari amewasili nchini humo kutetea ubingwa wake akiambatana na msaidizi wake Drew Sturrock.

  Madereva wengine waliowasili kushiriki ni kutoka Tanzania dereva Dharam Pandya atakayetumia gari aina ya Subaru Impreza pamoja na Dkt Gurvinder Bala, Charlie Lubega kutoka Kenya, Willie de Plessis toka Afrika Kusini na Leroy Gomes wa Zambia na mwenyeji Mafu mafu Lwakataka.

  Mashindano hayo yatakuwa ya mizunguko mitano, yakianzia mjini Busiika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako