• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Ulaya zakubaliana kuendelea kuunga mkono makubaliano ya nyuklia ya Iran

    (GMT+08:00) 2019-08-02 08:55:38

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amekutana na mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia diplomasia na sera za usalama Bi. Federica Mogherini mjini Bangkok, Thailand.

    Pande hizo mbili zimebadilishana maoni kuhusu masuala ya Iran, Afghanistan na masuala mengine ya kikanda na ya kimataifa, na kukubaliana kuendelea kuunga mkono makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA, kulinda mfumo wa pande nyingi na biashara huria, na kupinga uwekaji vikwazo bila sababu maalum.

    Habari zinasema, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imetoa taarifa kuwa, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zinapinga vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako