Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia ameukana uraia wake wa Marekani, japo nchi hiyo inamruhusu kuwa na uraia wa nchi mbili. Rais huyo amesema hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa taratibu zinazohitajika za kisheria na za uhamiaji baada ya uchaguzi wa rais. Rais Farmajo aliyechaguliwa kuwa rais wa Somalia Februari 2017 aliishi, kupata elimu na kufanya kazi nchini Marekani. Aliwahi kuwa waziri mkuu wa Somalia kuanzia Novemba mwaka 2010 hadi Juni mwaka 2011.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |