• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawataka wakulima kuzingatia kilimo cha kisasa

    (GMT+08:00) 2019-08-02 18:43:09

    Serikali ya Tanzania imewahimiza wakulima nchini humo kuzingatia kilimo cha kisasa kitakachosaidia kukuza kipato chao.

    Kauli hiyo ilitolewa na naibu waziri wa kilimo Bw. Hussein Bashe alipotembelea banda la Benki ya CRDB kwenye uzinduzi wa maonyesho ya 29 ya Nanenane.

    Bashe ameipongeza benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kuwawezesha wakulima na wajasiriamali waliopo kwenye sekta ya kilimo kwa mikopo ya aina mbalimbali inayotoa.

    Ameongeza kuwa kwa kutumia huduma za benki, itasaidia kuboreha uzalishaji na kuongeza tija ya shughuli za wakulima hivyo kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi

    Katika maonyesho hayo, Benki ya CRDB kwa kushirikiana na kampuni ya ETC Agro inatoa mikopo ya pembejeo za kilimo yakiwamo matrekta.

    Mkurugenzi wa wateja wadogo na wa kati wa CRDB, Boma Raballa amesema wamejipanga vyema kusaidia kujenga uchumi imara kwa kuimarisha sekta ya kilimo kinachotegemewa kwenye mnyororo wa uzalishaji bidhaa za viwandani.

    Zaidi ya asilimia 40 ya mikopo inayotolewa na CRDB nchini humo inaelekezwa kwenye kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako