Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inasikitishwa na inapinga hatua ya Marekani ya kujitoa kwenye Mkataba wa makombora ya masafa ya Kati (INF).
Ameeleza kuwa hiki ni kitendo kingine cha Marekani cha kupuuza ahadi za kimataifa ilizozitoa, na kufuata utaratibu wa upande mmoja, hali itakayopunguza kuaminiana kwa usalama wa kimkakati duniani, na kuleta matishio mapya kwa utaratibu wa usalama wa dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |