• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema China inapinga Marekani kuongeza ushuru wa bidhaa za China kuingia Marekani

  (GMT+08:00) 2019-08-02 20:18:28

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema kuwa kitendo cha Marekani kuongeza asilimia 10 za ushuru wa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 300, kimekwenda kinyume na makubaliano ya mkutano wa mazungumzo ya marais wa nchi hizo mbili, kutonufaisha utatuzi wa mgogoro, na China inapinga vikali.

  Bi. Hua ameongeza kuwa kama Marekani ikatekeleza hatua za kuongeza ushuru, China haitakuwa na budi kuchukua hatua dhidi ya kitendo hicho, na kulinda maslahi yake, na majadiliano yoyote yatatakiwa kufanyika katika msingi wa usawa na kuheshimiana, na matokeo yoyote ya majadiliano yanatakiwa kuwa ya kunufaishana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako