• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalam wa nchi za nje waliotembelea Xinjiang wasifu masikilizano na utulivu wa mkoa huo

  (GMT+08:00) 2019-08-03 18:09:46

  Wataalamu na wasomi kutoka nchi za nje waliofanya matembezi mkoani Xinjiang wamesifu utulivu na masikilizano katika jamii, na ustawi na maendeleo ya kiuchumi mkoani humo.

  Francesca Manenti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kimataifa cha Italia amesema amejionea maendeleo ya Xinjiang na masikilizano ya kijamii, na kwamba hasara kubwa zilizotokana na matukio ya kigaidi yaliyotokea mkoani Xinjiang zinafanana na zile ilizopata Ulaya miaka kadhaa iliyopita.

  Alipotembelea maonyesho ya kesi za kigaidi zilizotokea mkoani Xinjiang, mtafiti wa taasisi ya Schiller ya Ufaransa Rutte Anbeidon, amesema hakuna dini au maadili yoyote yanayoruhusu vitendo viovu kama hivyo, na amaetoa wito kwa nchi mbalimbali kupambana na ugaidi unaoathiri dunia nzima na binadamu wote. Ameongeza kuwa katika miaka hii mitatu, hakuna matukio ya kigaidi yaliyotokea Xinjiang, na katika kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi, aliona wanafunzi wanajifunza ufundi, pia wanaimba na kuchora."

  Mkuu wa shirika la kiraia la Poland, Polish House, Bw. Adam Ludwichak amesema katika maongezi yake na wanafunzi wa kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi, anasema ni ukweli unaweza kuzuia uwongo na anaweza kuwaona wao wakiishi kwa furaha.

  Naye mchambuzi na mtangazji wa televisheni ya taifa ya Pakistan Sultan Mahmoud Harry, amesema katika msikiti alijionea jinsi serikali ya China inavyoheshimu uhuru wa watu wa kuadubu, kuona waislamu wanafunga katika mwezi mtukufu wa ramadhani na hali halisi kuhusu "itikafu". Anaona serikali ya China inapambana na matukio ya kigaidi huku ikitatua masuala ya itikadi kali kutoka kwenye mzizi kwa njia ya maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako