• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Marekani asema sera ya "nchi moja, mifumo miwili" ya Hong Kong inalingana na maslahi ya jamii ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-08-03 18:10:23

    Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai amesema ustawi wa Hong Kong unaendana na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Cui amesema hayo katika makala aliyoitoa katika jarida la Newsweek la Marekani yenye kichwa cha "kushikilia 'nchi moja, mifumo miwili', kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong". Amesema "nchi moja, mifumo miwili" ni sera ya China, sio sera ya Marekani au Ulaya, na jaribio la kuilazimisha Hong Kong ifuate sera ya nchi nyingine sio tu ni changamoto kwa nchi moja, bali pia linaharibu "mifumo miwili". Bw. Cui amenukuu mfululizo wa takwimu akithibitisha kuwa kutokana na sera ya "nchi moja, mifumo miwili", uchumi wa Hong Kong umekua baada ya eneo hilo kurudi China, na kwamba thamani ya uzalishaji wa jumla GDP katika eneo hilo kwa mwaka 2018 ilikuwa dola za kimarekani bilioni 360, ambacho ni mara mbili kuliko mwaka 1996.

    Bw. Cui amesema watu wenye nia mbaya wa ndani au nje ya Hong Kong wanaitumia eneo hilo kama sehemu ya kwanza ya kushambulia sera za China bara na hata kuvuruga China nzima, na hawajali maisha ya wakazi milioni 7 wa Hong Kong. Amesisitiza kuwa masuala ya Hong Kong ni masuala ya ndani ya China, na China kamwe hairuhusu nchi yoyote kuingilia.

    Habari nyingine zinasema polisi wa Hong Kong wamewakamata watu wanane kutokana na umiliki wa silaha na vifaa vya milipuko katika operesheni yao katika jengo la kiviwanda huko Fo Tan, New Territories. Watu hao wakiwemo wanaume saba na mwanamke mmoja akiwemo Chan Ho-tin, mwitishaji wa "Chama cha Taifa cha Hong Kong" kilichopigwa marufuku kwa mujibu wa sheria, wanatuhumiwa kuhusika na mfululizo wa matukio ya kimabavu yaliyotokea hivi karibuni huko Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako