• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Hong Kong yalaani matukio ya kimabavu ya waandamanaji wenye msimamo mkali

  (GMT+08:00) 2019-08-04 17:09:00

  Serikali ya mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong imesema polisi waliwakamata waandamanaji 20 wenye msimamo mkali wanaotuhumiwa kukusanyika kinyume cha sheria, kushambulia ofisi ya polisi, kuharibu magari na kuchoma moto sehemu mbalimbali.

  Msemaji wa serikali amesema vitendo vya uhalifu vinavyotokea hivi karibuni katika maandamano ya kueleza madai vinazidi kuongezeka na ni tofauti na uhuru wa kuongea uliopo katika jamii ya ustaarabu. Amesema polisi wa Hong Kong watatekeleza sheria ipasavyo na kuwachukulia hatua za kisheria waandamanaji wanaokiuka sheria kwa kutumia mabavu, na wana uwezo na nia imara ya kulinda utulivu wa jamii.

  Wakati huohuo, Ofisi inayoshughulikia Masuala ya Hong Kong na Macao ya Baraza la Serikali la China na Ofisi ya Mawasiliano ya Serikali Kuu ya China huko Hong Kong, zimelaani vikali kitendo cha kutupa bendera ya taifa ya China baharini kilichofanywa na baadhi ya watu wenye msimamo mkali.

  Video iliyowekwa mtandaoni jana imeonyesha kuwa baadhi ya watu waliovaa nguo nyeusi walipanda mlingoti wa bendera uliopo karibu na Bandari ya Victoria ya Hong Kong, kuichukua kwa nguvu bendera ya taifa na kuitupa baharini.

  Naye Leung Chun-ying, naibu mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China alitoa zawadi ya dola za kimarekani 128,000 kwa watu wanaotoa taarifa zinazosaidia kukamatwa kwa waliofanya uhalifu huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako