• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 20 wameuawa na wengine 26 wamejeruhiwa katika jimbo la Texas.

    (GMT+08:00) 2019-08-04 17:24:58

    Tukio la mauaji ya watu wengi limetokea katika mji wa El Paso katika jimbo la Texas nchini Marekani na kusababisha vifo vya watu 20 na wengine 26 kujeruhiwa.

    Kamanda wa polisi wa jimbo la Texas Gerg Allen amemtaja muuaji kuwa ni kijana mzungu mwanaume mwenye umri wa miaka 21. Hata hivyo Shirika la upelelezi la Marekani FBI, limesema uchunguzi zaidi unatakiwa kufanyika ili kujua chanzo cha shambulizi hilo.

    Polisi wamesema mshambuliaji alifanya shambulizi kwenye duka la Walmart lililokuwa na wateja takriban 3000.

    Muda mfupi baadaye shambulizi lingine limetokea alfajiri mjini Dayton katika jimbo la Ohio, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 9 na wengine 16 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako