• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hamilton ashinda Grand Prix ya Hungary

  (GMT+08:00) 2019-08-05 10:29:14

  Lewis Hamilton amerejesha nguvu zake katika mabingwa wa dunia kwa kuweka ushindi wa kihistoria Jana Jumapili baada ya kumpita mshindani wake mchanga Max Verstappen ikiwa imesalia mizunguko mitatu kumalizika kwa mbio za langalanga katika mashindano ya Grand Prix ya Hungary. Hamilton mwenye miaka 34 na anayetetea kwa mara ya tano ubingwa wake, huu umekuwa ushindi wake wa saba nchini Hungary, na ukiwa wa nane kwa mwaka huu na wa 81 tangu aanze mbio za langalanga.

  Naye Mick Schumacher jana alijibebea ushindi wake wa kwanza kwenye Formula Two, ikiwa ni miaka 15 baada ya baba yake Michael kushinda mbio za Grand Prix za Hungary. Schumacher ni dereva wa Ferrari academy na inaaminika kwamba baadaye atahamia F1. Akiangaliwa na mama yake Corinna, Schumacher mwenye miaka 20 alionesha ustadi wake wa kudhibiti usukani na kupata ushindi mnono.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako