• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taifa Stars yasonga mbele kwenye hatua za kufuzu michuano ya CHAN kwa kuifunga Kenya goli 4 -1

  (GMT+08:00) 2019-08-05 10:29:38

  Ile kiu ya Taifa Stars ya Tanzania kulipiza kisasi dhidi ya Harambee Stars ya Kenya sasa imekatika baada ya Taifa Stars kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua za kufuzu kushiriki michuano ya CHAN kwa kuibanjua Kenya kwa magoli 4 -1 baada ya kupigiana mikwaju ya penati. Hatua ya mikwaju ya penati imekuja baada ya timu hizo kutoka sare ya kutofungana ndani ya Dakika 90 za kawaida. Kwa matokeo hayo Tanzania inasonga mbele na Kenya wameshatolewa kwenye hatua ya kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya CHAN. Harambee Stars walitoka sare ya kutofungana Jumapili iliyopita mjini Dar es Salaam na kufuatia ushindi huo Taifa Stars sasa itakutana na Sudan katika raundi ya pili na ya mwisho ya kufuzu.

  Wakati huohuo timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa 8-0 dhidi ya Eswatini jioni ya jana Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini. Mara baada ya mchezo, huo nyota wa Tanzanite, Diana Msemwa alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora ikiwa mara ya pili mfululizo. Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Tanzania, baada ya Ijumaa kuichapa 2-0 Botswana Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth.

  Tanzanite itateremka tena dimbani Jumanne kumenyana na Zambia kukamilisha mechi zake za Kundi B. michuano hiyo iliyoanza juzi, itafikia tamati Agosti 11.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako