• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yves Nkurunziza ashinda mbio za baiskeli za Tour de Kigali

  (GMT+08:00) 2019-08-05 10:30:14

  Mwendesha baiskeli wa Rwanda Yves Nkurunziza Jumamosi alishinda sehemu ya pili ya Kombe la mbio za Baiskeli 'Tour de Kigali' la mwaka 2019 ambalo limeshuhudia waendesha baiskeli wakishindana katika mji wa Kigali. Mbio hizo ni makala ya pili baada ya mbio za 'Northern Challenge' zilizofanyika mwezi uliopita ikiwa ni sehemu ya Kombe la mbio za Baiskeli la Rwanda. Washindani walianza mbio zao huko Intwari, Nyamirambo, na kupita Nyakabanda, Kimisagara, Nyabugogo, Muhima, Yamaha, APACOPE, Gakiriro hadi Gitega. Katika kitengo cha vijana "junior category" Jeremy Ngendahayo alishinda mbio kwa kutumia saa 2 na sekunde 39, akifuatiwa na Elysee Bikorikana aliyetumia saa 2 dakika 44 na sekunde 32 seconds na Jean-Nepo Bigirimana akawa wa watatu kwa kutumia saa 2 dakika 44 na sekunde 51.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako