• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupanua masoko ya vijijini

    (GMT+08:00) 2019-08-05 16:59:59

    Mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu kazi za uchumi kwa nusu ya pili ya mwaka huu uliofanyika wiki iliyopita umetaka kupanua soko katika sehemu za vijijini. Wasomi nchini China wanasema, wakati China inapopanua mahitaji ya ndani ya nchi, hadhi ya masoko ya vijijini imeanza kuzingatiwa zaidi.

    Naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa uchumi mkubwa katika Chuo Kikuu cha Xiamen Lin Zhiyuan anaona kuwa, mkutano huo umeweka bayana sera kuhusu jinsi ya kupanua mahitaji ya ndani ya nchi, ikimaanisha kuweka kipaumbele katika manunuzi, ukisisitiza kufanya mageuzi kuongeza matumizi, na pia kupanua manunuzi katika sehemu za vijijini.

    Meneja wa kampuni moja ya mashine ya umeme Bw. Yang amesema, bidhaa za kampuni yake zinanunuliwa zaidi katika masoko ya vijijini. Anasema, "Mahitaji ya mashine ya kusafisha maji yameongezeka katika miaka ya hivi karibuni katika masoko ya vijijini, na kasi ya ongezeko inafikia zaidi ya asilimia 30. Kuna sababu kuu mbili, moja ni mahitaji ya mashine ya kusafisha maji vijijini ni makubwa kuliko sehemu za mijini kutokana na usafi wa maji, pili ni kuwa watu wanaoishi vijijini wana kiwango kikubwa zaidi cha kupokea bidhaa mpya."

    Kwa mujibu wa Idara ya Takwimu ya Taifa ya China, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, mapato yaliyotumiwa na mtu mmoja mmoja katika sehemu za vijijini nchini China yaliongezeka kwa asilimia 8.9 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho, na matumizi ya mkazi mmoja mmoja vijijini yaliongezeka kwa asilimia 8.7. Hivyo inafaa kwa sasa kwa serikali ya China kuwa na mpango wa kupanua masoko ya vijijini. Wasomi wanaona kuwa matumizi ya sehemu za vijijini za China yanaweza kuongezeka zaidi. Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa biashara ya kimataifa katika Taasisi ya Kamati ya Kuhimiza Biashara ya China Zhao Ping anasema, matumizi ya bidhaa katika sehemu za vijijini za China hayajafikia asilimia 15 ya yale ya jumla nchini China, lakini idadi ya watu waishio vijijini imefikia karibu asilimia 40 ya watu wote. Ndio maana asilimia 40 ya watu wanachangia asilimia 15 ya matumizi nchini, hii inamaanisha kuwa kutakuwa na ongezeko jipya la matumizi kama masoko ya vijijini yakipanuliwa.

    Utafiti umeonyesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, biashara iliyofanywa katika mitandao wa internet iliongezeka kwa kasi zaidi katika sehemu za vijijini za China, na wakulima wengi wanapenda kufanya manunuzi mtandaoni. Bibi Wang ni mmoja wao, na alikuwa na haya ya kusema, "Zamani, ilitubidi tuchukue vifurushi katika kitongoji, lakini sasa kila kijiji kina kituo cha kupokea vifurushi, ni rahisi sana, na hata tunaweza kupokea nyumbani moja kwa moja."

    Mbali na hayo, wasomi wengi wanaipendekeza serikali kuhamasisha kampuni kutengeneza bidhaa zinazofaa zaidi masoko ya vijijini. Mtafiti wa idara ya utafiti wa maendeleo ya vijijini ya Taasisi ya Sayansi Jamii ya China Li Guoxiang ana pendekezo kama hilo. Anasema, "Kampuni zinazolenga kupanua masoko ya vijijini zinapaswa kutengeneza bidhaa zinazofaa hali tofauti za vijiji vya sehemu mbalimbali. Ni kweli wanavijiji wanataka kumiliki bidhaa walizo nazo watu waishio mijini, lakini wana hali tofauti katika matumizi. Ndiyo maana, kampuni zinazopanua masoko vijijini, zinapaswa kuzingatia tofauti hii."

    Ili kupanua matumizi katika sehemu za vijijini, baraza la serikali la China limetaka biashara ya kielektroniki ifanyike katika maeneo zaidi ya vijijini, na kutatua tatizo lililopo sasa la usafirishaji wa mazao ya kilimo unaohitaji mazingira baridi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako