• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli yaunganisha pwani za mashariki na kusini magharibi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-08-05 20:14:48

    Treni ya kifahari iliyobeba watalii zaidi 50 imefunga safari kutoka Lobito, mji wa bandari wa Angola kupitia reli ya Benguela na kurudi Dar es Salaam, Tanzania. Hii inamaanisha kuunganishwa kikamilifu kwa reli ya kwanza kati ya pwani za mashariki na kusini magharibi barani Afrika.

    Ikiwa ni sehemu ya reli hii nzima, reli ya Benguela inapita kwenye nchi nzima ya Angola na ilijengwa na kampuni ya CREC ya China. Reli hiyo imeungana na reli ya TAZARA iliyojengwa na China katika miaka ya 70 karne iliyopita. Treni hiyo itasafiri umbali wa kilometa 4,300 ikipita Tanzania, Zambia, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Angola.

    Reli hii inaonekana kuwa njia muhimu ya kuhimiza maendeleo ya uchumi na utalii kwenye sehemu karibu na reli hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako