• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Manchester United yamalizana na Maguire, awa beki ghali duniani, pini miaka sita

  (GMT+08:00) 2019-08-06 08:18:52

  Harry Maguire anaingia kwenye rekodi ya mabeki ghali duniani baada ya usajili wake kukamilika na Manchester United kuthibitisha kuwa wametumia pauni milioni 80 likiwa ni dau la usajili wake kutoka Leicester City. Akiwa mchezaji rasmi wa Manchester United Maguire amesaini mkataba wa miaka sita. Usajili huo unamfanya nyota huyo kuwa beki wa thamani zaidi duniani na atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki. Baada ya kunaswa Maguire aliuambia mtandao wa klabu ya Manchester United kwamba amefurahi kusajiliwa katika klabu kubwa. Na kwamba alikuwa na wakati mzuri alipokuwa na Leicester City. Ni wazi kwamba kocha Ole yupo katika mipango kabambe ya kutengeneza kikosi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako