• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyota wa kikapu apigwa marufuku baada ya vipimo kuonesha ni  mjamzito

    (GMT+08:00) 2019-08-06 08:19:59
    Mcheza kikapu wa Marekani DJ Cooper amepigwa marufuku ya kushangaza katika kumbukumbu za hivi karibuni. Cooper aliondoka AS Monaco mwishoni mwa 2018 kutokana na sababu za kifamilia, na kujaribu kujiunga na timu ya taifa ya Bosnia. Hata hivyo hakufanikiwa na badala yake akakabidhiwa zawadi ya marufuku ya miaka miwili kutoka FIBA baada ya kupimwa kama anatumia dawa za kuongeza nguvu au la. Lakini kwa upande wa Cooper hakupigwa marufuku kwa dawa za kusisimua misuli, bali baada ya kupimwa alionekana ni mjamzito. Vipimo vya haja ndogo alivyowasilisha Cooper vinaonesha kuna uwepo wa hCG ambayo ni homoni inayotolewa na fuko la uzazi wakati wa ujauzito. Kulingana na ripoti mkojo aliowasilisha ulikuwa wa mpenzi wake ambaye hakujua kama ni mjamzito wakati huo. Hivyo, FIBA imempiga marufuku Cooper kwa udanganyifu. Kulingana na marufuku yake atarejea tena kucheza Juni 20, 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako