• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi 12 kushiriki kwenye mashindano ya World Tour Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-08-06 08:20:37
    Nchi 12 zimethibitisha kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa wavu wa ufukweni ya mwaka 2019 maarufu kama Beach Volleyball World Tour, ambayo yatafanyika kwa siku nne kuanzia Agosti 21 hadi 24 katika fukwe za Ziwa Kivu, Wilaya ya Rubavu nchini Rwanda. Kulingana na Mkurugenzi wa mashindano hayo ya Mpira wa wavu wa ufukweni, Christian Hatumimana, nchi hizo 12 ambazo zinashiriki kwenye vitengo vya wanawake na wanaume ni pamoja na: Cote D'Ivoire, Uingereza, Uholanzi, Slovenia, Denmark, Japan, Canada, Jamhuri ya Czech, Norway, Sweden, Cyprus na wenyeji Rwanda. Rwanda itatoa timu tatu kwa kila kitengo. Wiki iliyopita timu ya Rwanda ilianza maandalizi makali na itaingia kambini kesho Jumatano huko Rubavu. Ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika Afrika Mashariki na yatatumia bajeti ya Rwf million 350.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako