• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Sudan na Sudan Kusini wasaini makubaliano ya ushirikiano

  (GMT+08:00) 2019-08-06 19:37:31

  Polisi wa Sudan na Sudan Kusini wamesaini makubaliano ya ushirikiano ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  Makubaliano hayo yalisainiwa jana mjini Juba na makamanda wa polisi wa pande hizo mbili, kwa lengo la kuimarisha ujenzi wa uwezo, kubadilishana habari za kijasusi na kushughulikia visa wakati wa kuwasili kwa raia wa nchi hizo mbili.

  Ushirikiano huo pia unahusu kubadilishana taarifa kuhusu uhalifu wa kupangwa na ule wa kuvuka mipaka, na kufanya uratibu kwenye uungaji mkono kwenye mambo ya ugavi.

  Kamanda wa polisi wa Sudan Kusini Bw. Majak Akech amesema huu ni mwanzo na ni ishara ya nia njema ya jeshi la polisi la Sudan Kusini kwa jeshi la polisi la Sudan. Pia amesema wamefurahishwa kushirikiana na Sudan na kutumai kuwa ushirikiano huo utakuwa ni wa muda mrefu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako