• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Safaricom nchini Kenya imewekeza dola milioni 4 kwenye M-pesa global

    (GMT+08:00) 2019-08-06 19:57:10

    Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom nchini Kenya imewekeza dola milioni 4 katika huduma yake ya kutuma na kupokea pesa kimataifa ikiwa ni mojawepo wa juhudi zake za kukuza zaidi matumizi ya huduma M-Pesa.

    Safaricom inasema huduma yake ya M-Pesa Global, ilishughulikia shilingi bilioni 101 katika kipindi kilichokamilika Machi 2019.

    Huduma hiyo inawezesha wateja kutuma na kupokea fedha, kulipa na kufanya biashara kwa kushirikiana na huduma nyingine kama vile Western Union, PayPal na AliExpress.

    Kulingana na taakwimu za Safaricom, mapato ya M-pesa yaliongezeka kwa asilimia 19.2 katika kipindi cha fedha kilichokamilika Machi 2019 ukiwa ni ukuaji wa haraka zaidi kuliko huduma nyingine za kampuni hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako