• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia na Marekani zaimarisha operesheni dhidi ya Al Shabaab

    (GMT+08:00) 2019-08-06 20:55:28

    Somalia na Marekani zimekubaliana kuimarisha operesheni za usalama ili kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab nchini Somalia.

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia mambo ya kisiasa Bw. David Hale, ambaye jana alikutana na waziri mkuu wa Somalia Bw. Hassan Ali Khaire mjini Mogadishu, alisema watayaandaa majeshi ya Somalia kuchukua nafasi ya kikosi cha tume ya Umoja wa Afrika.

    Marekani imesema kwenye taarifa kuwa pande mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa operesheni za usalama kuyakomboa maeneo kutoka mikononi mwa kundi la Al Shabaab.

    Bw. Khaire pia amemwambia ofisa huyo wa Marekani kuwa maendeleo ya hivi karibuni ya kisiasa na usalama, na maendeleo ya Somalia kukaribia kukidhi vigezo vya kupunguziwa deni, ambayo yatairuhusu Somalia kuanza kukopa tena kwenye taasisi za fedha za kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako