• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mali yavishwa taji laMabingwa wa FIBA U-16

  (GMT+08:00) 2019-08-07 08:35:00

  Timu ya mpira wa kikapu ya vijana wa kike walio chini ya miaka 16 ya Mali imefuzu kushiriki michuano ya mabingwa wa dunia chini ya miaka 17 itakayofanyika mwakani, baada ya Jumamosi usiku kushinda kombe la mabingwa wa Afrika kwa wachezaji wa kike chini ya miaka 16 FIBA katika kiwanja cha Amahoro. Mali imeishinda Misri katika mchezo wa fainali kwa vikapu 84-48 na kubeba taji hilo kwa mara ya sita. Baada ya kushinda katika nafasi mbili za juu Mali na Misri zimejikatia tiketi ya michuano ya mabingwa wa dunia chini ya miaka 17. Mariam Coulibaly aliyepachika vikapu 30 ametajwa kama Mchezaji Mwenye Thamani zaidi kwenye mashindano hayo na kujiunga katika All Star Five pamoja na wachezaji wengine wakiwemo Sara Caetano (Angola), Maimouna Haidara (Mali), Malak Sadek (Egypt), na Maria Najjuma (Uganda). Wakati huohuo Angola iliishinda Msumbiji kwa vikapu 67-59 na kuchukua nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako