• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema uamuzi wa Marekani wa kuiorodhesha kuwa nchi inayodhibiti thamani ya sarafu yake ni wa makosa

    (GMT+08:00) 2019-08-07 08:56:11

    Kaimu Gavana wa Benki Kuu ya Watu wa China (PBOC) Chen Yulu amesema, uamuzi wa Wizara ya Fedha ya Marekani wa kuiorodhesha kuwa nchi inayodhibiti thamani ya sarafu yake sio sahihi.

    Amesema uamuzi huo sio tu unakiuka mwafaka wa kiuchumi na kimataifa, lakini pia unashindwa kufikia kigezo kwa kile kinachoitwa "nchi inayodhibiti thamani ya sarafu yake" kilichowekwa na wizara ya fedha ya Marekani.

    Chen amesema, China haijawahi kushusha thamani ya sarafu yake ili kuongeza ushindani na kamwe haitatumia fedha kama nyenzo ya ushindani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako