• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yeleza msimamo wake kuhusu Marekani kujitoa INF

    (GMT+08:00) 2019-08-07 09:03:11

    Balozi wa China anayeshughulikia mambo ya kupunguza silaha Bw. Li Song ameeleza msimamo wa China kuhusu Marekani kujitoa kwenye Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati INF.

    Bw. Li Song amesema hayo jana kwenye mkutano wa mazungumzo ya kupunguza silaha. Amesema China inasikitishwa na hatua hiyo ya Marekani ambayo haikutilia maanani upinzani uliotolewa na jumuiya ya kimataifa. Amesema hatua hiyo ya upande mmoja ya Marekani isiyo ya kuwajibika, itaathari uwiano na utulivu wa kimkakati wa dunia, kuongeza hali ya wasiwasi ya uhusiano wa kimataifa, kuvunja uaminifu kati ya nchi kubwa, kuathiri mchakato wa kupunguza na kudhibiti silaha za nyuklia, na kutishia amani na usalama wa maeneo husika.

    Bw. Li Song ameitaka jumuiya ya kimataifa kufuatilia kwa makini athari mbaya zitakazojitokeza kwa Marekani kujitoa INF, na kuizuia Marekani kukwepa wajibu wake wa kupunguza silaha za nyuklia kwa kisingizio chochote. China inaitaka Marekani kujizuia, na kutochukua hatua zitakazodhuru maslahi ya usalama ya nchi nyingine, kulinda amani na usalama wa dunia nzima na ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako