• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China atoa salamu za rambirambi kutokana na shambulizi la kigaidi nchini Misri

  (GMT+08:00) 2019-08-07 17:22:49

  Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Misri Bw. Abdel-Fattah al-Sisi kutokana na shambulizi la kigaidi lililotokea nchini humo.

  Kwenye salamu hizo, rais Xi amesema kwa niaba ya serikali na watu wa China ameomboleza vifo vya watu waliouawa kwenye shambulizi la mabomu, kutoa salamu za rambirambi kwa majeruhi na wafiwa, na kuwatakia majeruhi wapone haraka. Amesisitiza kuwa China inapinga aina zote za ugaidi na kulaani vikali shambulizi hilo. Pia amesema China itaendelea kuiunga mkono Misri kulinda usalama na utulivu wa nchi na jitihada za kupambana na ugaidi.

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa taarifa kulaani vikali shambulizi hilo la mabomu la gari lililotokea usiku wa tarehe nne mjini Cairo na kusababisha vifo vya watu 20 na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako