• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuiorodhesha China kuwa nchi inayodhibiti kiwango cha safaru yake ni siasa ya kujichukulia maamuzi ya upande mmoja

    (GMT+08:00) 2019-08-07 18:02:22

    Wizara ya Fedha ya Marekani imeiorodhesha China kuwa inadhibiti kiwango cha sarafu yake. Hii sio tu hailingani na vigezo vilivyowekwa na Wizara hiyo vya "nchi inayodhibiti kiwango cha sarafu", bali pia ni siasa ya kujichukulia maamuzi ya upande mmoja na kitendo cha kujilinda kibiashara. Hatua ambayo itaharibu vibaya kanuni za kimataifa na kuleta athari kubwa kwa shughuli za uchumi na fedha duniani.

    Mwezi Mei mwaka huu, Wizara ya Fedha ya Marekani ilitoa ripoti ikisema kwa mujibu wa vigezo vitatu ilivyoweka, China inakidhi kigezo kimoja tu cha "pengo la biashara na China linazidi dola za kimarekani bilioni 20 kila mwaka", hivyo haihesabiwi kuwa nchi inayodhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu kwa ajili ya kujipatia faida isiyo ya haki. Hata hivyo miezi miwili baadaye, Wizara hiyo imeligeuza uamuzi wake, kauli zake zinakinzana na kuinafuata sera ya kuangalia manufaa ya wakati huu.

    Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na Shirika la Biashara Duniani na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, IMF ni chombo maalumu cha kimataifa cha kusimamia kiwango cha ubadilishaji wa sarafu, na maoni yake ya kitaaluma ni sharti la kwanza na ni msingi wa kuamua nchi fulani inadhibiti kiwango cha sarafu au la, na Marekani haina madaraka hata kidogo ya kutathmini kiwango cha sarafu cha nchi nyingine. Katika majadiliano yaliyomalizika hivi karibuni, IMF ilisema kiwango cha sarafu ya China Yuan kinaendana na misingi ya uchumi wake.

    Tangu mwanzo wa mwezi Agosti mwaka huu, thamani ya Yuan ilishuka kwa kiasi, na hii inatokana na vitendo vya kujichukulia maamuzi ya upande mmoja na kujilinda kibiashara na makadirio yna Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China, na ni matokeo halisi ya hali ya utoaji na mahitaji sokoni na kubadilika kwa soko la hisa duniani. Ikiwa nchi inayoshika nafasi ya pili duniani kwa nguvu ya kiuchumi, China siku zote inafuata ahadi kuhusu suala la kiwango cha safaru katika mikutano mbalimbali ya viongozi wa kundi la G20, na hata baada ya Marekani kuanzitisha vita ya kibiashara na China mwaka 2018, China haijachukua hatua ya imekuwa ikiacha kitendo cha kushusha thamani ya sarafu yake, na haijawahi kutumia kiwango cha sarafu kama ni njia ya kukabiliana na mgogoro wa kibiashara.

    Lengo la Marekani kuitaja China kuwa nchi inayodhibiti kiwango cha sarafu ni kuendelea kuweka ishinikizao kwa China, kuvurugasumbua makadirio ya soko na kupunguza nguvu ya uchumi wa China.

    Siku zote, Benki Kuu ya China imelinda utulivu wa kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya ChinaYuan. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya Kimataifa ya BIS, kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2005 hadi mwezi Juni mwaka huu, thamani ya sarafu ya China Yuan iliongezeka kihalisia kwa asilimia 47, ni sarafu yenye nguvu zaidi katika nchi za kundi la G20, pia ni moja kati ya sarafu ambazo thamani zake zinaongezeka zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako